Thursday, June 14, 2012
KASHIFA NZINTO KWA WATENDAJI BIHARAMULO
Na
Magreth
Chaba
Biharamulo
MADIWANI wa
Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wametishia kumunganisha mwenyekiti wao kwenye tuhuma zinazomkabili
mweka hazina wa halmasauri hiyo baada ya kubaini kiasi cha
sh.mill.101.8kutojulikana matumizi yake kufuatia kamati maalum iliyoiundwa
februari 14,mwaka huu kuchunguza matumizi ya fedha za halmashauri hiyo.
Hatua hiyo
ilikuja kufuatia mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Apolinal Mugarura kuonyesha
wazi wazi kumlinda mweka hazina huyo,Alexanda Bashaura na kuwabania madiwani
kuchangia hoja za kamati hiyo zilizowasilishwa kwenye baraza hilo baada ya
kamati yao kubaini utofauti wa zaidi ya sh.101.8 mill kwenye akaunti za
halmashauri hiyo.
Akichangia hoja ya taarifa ya kamati teule ya madiwani,diwani
viti maalumu Zayun Husein alisema,mbali na fedha hizo kutoonekana matumizi yake
mwenyekiti alionekana kumlinda mweka
hazina na hivyo kudai kuwa kama ataendelea kumtetea na yeye watamuunganisha
kwenye tuhuma hizo ili achunguzwe.
‘’Kama fedha hizo zinaonekana kuliwa na wewe mwenyekiti
unaonekana unawatetea hawa watuhumiwa,tutakuunganisha na wewe kwenye tuhuma
hizi za mweka hazina maana unaonekana kutubania sisi kuchangia hoja zetu,kwa
hiyo na wewe uchunguzwe…hatuwezi kutetea upovu wa fedha hizi’’alisema Husein.
Kauli ya diwani huyo iliungwa mkono na madiwani wote bila
kujali itikadi ya vyama vyao kwa maslahi ya kutetea fedha za umma kwa maendeleo
ya miradi ya wananchi,ambapo mwenyekiti huyo alisema yuko tayari kuunganishwa
kwenye tuhuma hizo na pia yuko wazi kuchunguzwa na kamati hiyo.
Akiwasilisha hoja za uchunguzi mwenyekiti wa kamati ndogo iliyo undwa na baraza hilo
Josephat Kayamba alisema,kutokana na uchunguzi wa kamati hiyo,kamati ilibaini
kiasi hicho cha fedha baada ya kukuta kuna kasoro nyingi kwenye akaunti tano za
halmashauri hiyo kati ya akaunti 32.
Kamati hiyo ya madiwani watano wakati wa uchunguzi wake
ilikutana na kuwahoji watumishi watano wa halmashauri hiyo akiwemo mkurugenzi
mtendaji Alhaji Zuberi Mbyana,mweka hazina,Mwanasheria ,mwenyekiti wao,mwaandishi
wa vikao vya halmashauri hiyo pamoja na
meneja wa benki ya NMB Norbert Mwenga.
Kayamba alisema kamati ilichunguza kwa kina akaunti zote na
kubaini tofauti kubwa katika akaunti tano za idara ya ardhi,tasaf,mamlaka ya
maji ya mji wa Biharamulo,mfuko wa barabara na ukimwi na kugundua kuwepo kwa
sh.101.8 kwenye benki kiasi ambacho kilitofautiana na taarifa iliyowasilishwa na
mweka hazina kwenye kikao cha mwezi februari.
Taarifa hiyo ya kamati ya ilionyesha kuwa kiasi cha fedha
iliyowasilishwa na mweka hazina mbele ya kikao cha baraza la madiwani kilichopita kilionyesha
kwenye akaunti hizo kuna sh.66.3 mill na kiasi halisi kilichoonekana kwenye
akaunti baada ya uchunguzi kufanyika kulionekana kuwa na sh.168.1 na hivyo
kamati kubaini utofauti wa sh.101.8 fedha
ambayo haijulikani matumizi yake.
Akijibu tuhuma hizo mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo Alexnda Bashaura amekiri kuwepo kwa tofauti ya fedha alizokuwa amezitolea
taarifa ukilinganisha na taarifa ya uchunguzi wa wa kamati iliyo undwa na
baraza hilo,na kudai kuwa taarifa hiyo imetofautiana kutokana na kwamba wakati
anatoa taarifa hiyo kulikuwa fedha nyingine iliyokuwa imeingizwa kwenye akaunti
hiyo kutoka hazina makao makuu fedha ambayo hakuwa na taarifa zake
Aidha Bashaura alisema kuhusu mchanganuo wa fedha hizo wakati
akitoa taarifa hizo alidai kutumia vitabu vya malipo[cashebook]na si mizania ya
banki[bankstatimate]zilizotumiwa na kamati ya madiwani baada ya kufuatilia
taarifa hizo benki kwa kupitia akaunti zote za halmashauri hiyo.
Pia mweka hazina huyo alifafanua,kuwa taarifa ya vitabu vya
fedha vinatofautiana na ripoti za benki
kutokana na kwamba fedha zimekuwa zikiingizwa kutoka hazina makao makuu Dar es
Salaam bila taarifa na hivyo kupelekea kuwepo kwa mkanganyiko mkubwa wa hesabu
za kifedha.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
Alhaji Zuberi Mbyana ameiomba ofisi ya katibu tawala mkoa Kagera kuunda tume ya
uchunguzi wa akaunti hizo ili waweze kuondoa utata na mkanganyiko wa matumizi
ya fedha hizo.
Hata hivyo madiwani hao wameiagiza tume hiyo itakayo undwa na
mkoa kuchunguza kwa kina akaunti hizo ikiwa ni pamoja na kuonyesha muda na siku
wa kuingia kwa fedha hizo ili waweze kubaini kama kuna ubadhirifu juu ya fedha
hizo.
MWISHO
MADIWANI BIHARAMULO WALITUHUMU JESHI LA POLISI
Na
Magreth Chaba
Biharamulo
MADIWANI
wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamelituhumu jeshi la
polisi wilayani humo kujihusisha na uharibifu wa mazingira baada ya kufumbia
macho vitendo vya uvushwaji wa mkaa na magogo ya miti(Mbilimbi) kinyume cha
sheria,ambapo mazao hayo husafirishwa na watu wanaosadikiwa wahamiaji haramu wa
nje ya nchi na kuyapeleka nchini Rwanda.
Askari
waliotuhumiwa ni wa kituo kidogo cha Nyakanazi wilayani humo ambapo wanadaiwa
kushirikiana na wavunaji haramu wa raslimali ya misitu kutoka nchini Rwanda
ambao huvusha mazao hayo kwa njia ya malori kupitia kizuizi kilichopo kwenye
kituo hicho cha polisi licha ya kujua wazi kuwa kufanya hivyo ni kuhujumu
uchumi wa taifa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya diwani wa kata ya Kalenge Gabriel Kakulu kutaka kujua
chanzo cha uharibifu mkubwa wa misitu katika msitu wa hifadhi ya taifa wa
Biharamulo upande wa kata ya Nyantakara ambapo eneo kubwa limeharibiwa vibaya
baada ya wavamizi wa ndani na nje ya nchi kuingia ndani yake kinyume cha sheria
na kujihusisha na ukataji miti ya kupasua mbao,uchomaji mkaa,kilimo na
uchimbaji madini.
Kutokana
na hali hiyo Kakulu alidai kutokuwa na imani na baadhi ya watendaji wa idara ya
misitu waliopo kwenye kata hiyo pamoja na jeshi la polisi wilayani humo
kushindwa kudhibiti uvushwaji wa mazao hayo kinyume cha sheria licha ya
mazao hayo kusafirishwa kupitia kizuizi cha polisi kilichopo jirani kabisa na
kituo kidogo cha Nyakanazi ambapo yamekuwa yakipelekwa nchini Rwanda pasipo
kutozwa ushuru hali inayopelekea halmashauri hiyo kupoteza mapato mengi kila
kukicha.
Subscribe to:
Comments (Atom)